CrucifixCatholic Diocese of Zanzibar

 

 

 

History

Bishop

Diocesan News

Diocesan Offices

Parishes

Schools

Sisters in Services

Contacts

Home

Links

 

Habari

JIMBO KATOLIKI LA ZANZIBAR

 

Ziara ya Baba Askofu Florida Marekani

Jengo la Parokia ya Kitope lahitaji kazi kubwa 

Askofu akutana na Mkuu wa mtandao (Webmaster)

Padre Ambrose Atembelea Kanisa la Mt. Benedict Florida

Padre Evaristus Mushi katika mlo wa hisani (mchango)

Askofu Augustine Saho na Padre Thomas Assenga wakiwa Minesota

Matukio Makuu Katika Mwaka 2005

Tamasha la watoto wa HAKI NA AMANI lilifanyika Tomondo tarehe 6 hadi 7 Januari 2005. Majimbo manne kutoka bara yalishiriki katika tamasha hili na kulifanya kuwa na sura ya kitaifa. Watoto walioshiriki wakisindikizwa na walezi wao pamoja na mapadre na masista wanahusika na PMS majimbini mwao ni kutoka:

Jimbo la Iringa,Jibo la Morogoro, Jimbo la Geita  

Jimbo la Njombe.

 Aidha mhashamu Baba Askofu Tarsisius Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa alikuwa Askofu pekee aliyetoka bara                

        kushirikiana na Askofu mwenyeji wa hapa visiwani Augustino Shao kwenye       tamasha hili.

     Tamasha lilikuwa limeandaliwa kitaifa; yaani kujumuisha mahjimbo yote ya Tanzania lakini baadaye ulitokea uamuzi kuwa majimbo ya bara hayawezi kushiriki kwa kuwa Zanzibar hakuna Amani ya kutosha. Kwa upande wa watoto waliohudhuria kutoka majimbo manne ya bara waliweza kushirikiana na watoto wenzao hapa Zanzibar na kuonyesha vipaji vyao kwa njia ya nyimbo, na michezo mbalimbali. Pia kuja kwao kulitufariji sana.

     Mhashamu Baba Askofu Augustino Shao alikwenda kwenye mafungo pamoja na jumuiya ya wanashirika la Roho Mtakatifu yaliyoaanza tarehe 16.Januari 2005.

     Januari 28 – 3 0, Mhashamu Baba Askofu Augustino Shao alihudhuria kusimikwa kwa Ashoku wa Jimbo la Tunduru masasi.

Jumatano ya Majivu 9. Fer. 2005 kipindi cha kwaresima kilianza na msisitizo mkubwa wa kuwataka waamini kufunga, kusali na kutoa saadaka. Hiki ni kipindi cha matayarisho kwa sikukuu ya Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu – Pasaka.

Mkutano wa Mapadre  ufanyika katika kanisa la Minara Miwili tarehe 14.02.05

 Askofu alifanya safari ya kumtembelea Baba Mtakatifu huko Roma inayojulikana kwa lugha ya kanisa kama “Adlimina” tarehe 7-18, March 2005

 Ibada ya Misa Takatifu ya kubariki mafuta ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu tarehe 21.03.2005. Siku hii pia mapadre walikuwa na muda wa pekee katika kutafakari. Baadaye jioni Mapadre na Masista walialikwa na Baba Askofu kwa mlo wa jioni.

 Siku ya Alhamisi Kuu (24.03.05) Baba Askofu aliadhimisha ibada ya Misa takatifu katika parokia ya Kitope.

 Sikuku ya Pasaka (27.3.2005) Baba Askofu aliadhimisha Misa ya Ufufuko katika Parokia ya Mpendae.

 Mhashamu Baba Askofu Augustino Shao alitoa Sakramenti ya Kipaimara katika parokia ya Machui 10.April 2005

 Mkutano ulifanyika Wete Pemba ambapo Baba Askofu alikutana na Watawa waume kwa wake wanaofanya kazi katika parokia za Wete na Chake. Lengo la mkutano huu lilikuwa kupanga mikakati ya kuboresha uinjilishaji katika kisiwa cha Pemba.

 Masista wa COLU hapa Zanzibar waliadhimisha Jubilee ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika lao. Kwa hapa Zanzibar sherehe hizi zilikwenda sambamba na ufunguzi wa jengo jipya la Masista wa COLU wanaofanya kazi katika parokia ya Kitope. Jengo hili linajulikana kama  “Ngawiliau’s Convent 2004” na ujenzi wake ulianza mwaka 2003.

Baba Askofu aliadhimisha Ibada ya Misa takatifu iliyofanyika Tomondo 15. 04.05 siku ya Pentekoste. Wakristu walihudhuria kwa wingi na walipata nafasi ya pekee ya kuhubiri. Mhashamu Baba Askofu Augustino Shao aliwasifu kwa mahubiri yao yaliyolenga katika kuifundisha jamii kuwa tayari kulitegemeza kanisa na kuona kuwa kanisa ni lao.

Mkutano Mkuu wa kichungaji ulifanyika Machui. Mkutano huu ulihudhuriwa na Mapadre, Masista, Halmashauri kuu ya Jimbo, makatekisata na viongozi wote wa vyama vya kitume hapa jimboni. Mkutano huu uligusia mada kuu zilizohusu Ukarabati wa Kanisa Kuu la Mt. Yosefu, Ujenzi wa Sekondari ya Marine ya Cheju pamoja na mada nyingine ndogondogo.

Baba Askofu alihudhuria Mkutano wa AMECEA uliofanyika Kampala Uganda 1-12, Juni 2005

Baba Akofu Augustino Shao alipokea taarifa za kusikitiksha kuhusu kifo cha Askofu Mtaafu Bernard Ngaviliau wa Jimbo la Zanzibar. Askofu mstaafu alikuwa akiumwa kwa kipindi kirefu na alifariki dunia katika hopoitali ya Mt. Theresia Arusha

siku ya Jumapili 26.Julai 2005. Askofu Bernard alikuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Zanzibar tangu 1980 – 1997 alipostaafu na nafasi yake ikashikwa na Mhashamu Askofu Augustino Shao. 

Ibada ya Misa takatifu kumwombea Askofu Mstaafu B. Ngaviliau ilifanyika katika kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu Zanzibar (6.Julai 2005).

Jumuiya ya mapadre na masista katika Kituo cha Hekima Cheju walimkaribisha baba Askofu ambaye alifanya ziara ya kichungaji kituoni hapo tarehe 22 – 24 Julai 2005.

Semina ya Viongozi wa WAWATA ilifanyika Mtoni tarehe 5 – 6 Augusti 2005. Semina hii iliyofunguliwa na Mhashamu Baba Askofu ilihusu “Nafasi ya Mama Mkatoliki katika Kanisa”. Pia WAWATA walipanga namna ya kuweza kuwasaidia watoto wanaosoma katika Kituo cha Malezi Cheju.

Walezi wa watoto wa Haki na Amani walikuwa na semina iliyofanyika Tomondo 17. Sptember 2005. Baba Askofu alifungua na kuendesha semina hii. Ilihusu mbinu mbalimbli katika kuwalea watoto wa Haki na Amani. Mratibu wa watoto wa Haki na Amani PMS, Sr. Rufina Funto alitayarisha semina hii akisaidiwa na walezi wa watoto wa Haki na Amani.

 Ziara ya Baba Askofu kutembelea vijana katika parokia zote za Unguja

     Ziara hii ya Baba Askofu katika parokia za Unguja ilikuwa na lengo la kukutana na vijana (UVIKAZA)  kushuhudia kazi zao za kitume na kufahamu juu la maswala muhimu yanayowahusu vijana hususani ukosefu wa ajira kwa vijana. Baba Askofu aliwataka vijana wawe mstari wa mbele katika shughuli za utume pamoja na shida nyingi walizo nazo kama ukosefu wa ajira na shida nyinginezo.  Aliwapa changamoto ya kuandaa sherehe za kufunga mwaka wa Ekaristi zitakazofanyika katika sikukuu ya Ekaristi Takatifu mwezi Juni 2006.

    Ratiba ya Baba Askofu kutembelea vijana ilikuwa kama ifuatavyo.

Ø      Kitope Parish 16. Oktoba 2005

Ø      Kizimbani 19. Oktoba 2005

Ø      Kiboje  21 na 23 Oktoba 2005

Ø      Kiembesamaki na vogango vya jirani 26.Oktoba 2005

Ø      Tomondo na Mpendae 28. Oktoba 2005

Ø      Maili sita na Kianga 15 Desemba 2005

Ø      Mbuzini 21. Desemba 2005

Semina ya UKIMWI iliyohudhuriwa na Mapadre na Masista ilifanyika Machui 21 Oktoba 2005.Semina hii ilihusu namna ya kuwahudumia walioathirika na VVU/UKIMWI hasa wale waliko majumbani. Pia semina ilielimisha kuhusu matumizi na upatikanaji wa dawa za kurefusha maisha kwa walioathirika tayari. Mtoa mada alikuwa ni Dr. Emmanuel Makanza na Mama anayefanya kazikatika kitengo cha UKIMWI hospitali ya Mnazi mmoja.

     (29 Oktoba 2005) Ibada ya Misa takatifu iliadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mt. Yosef Zanzibar kuombea uchaguzi ufanyike kwa amani, pia kuomba ili tupate viongozi wanaofaa kuliongoza taifa letu katika hali ya amani na utulivu. Uchaguzi ulifanyika kwa hapa Zanzibar 30 Oktoba 2005 na ulimalizika kwa amani. Tunamshukuru Mungu kwa amani tuliyo nayo na kuzidi kuomba ili amani hiyo izidi kudumu katika Taifa letu la Tanzania. Mungu ibariki Afrika – Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

     Novemba tarehe ya 2, ilifanyika Misa ya kuwaombea marehemu na baada ya Misa Mapadre walikuwa na Ibada ya kubariki Makaburi mbalimbali katika Parokia zote. Kipindi cha kwaresma kinaanza rasmi baada ya Jumatano ya Majivu. Ni kipindi cha pekee kwa wakristu ambapo hufunga, kutoa zaka, kusali na kutenda matendo mema.

     Mafungo ya mwaka kwa mapadre wote Unguja yalifanyika Machui kuanzia tarehe 23 hadi 19 Novemba 2005. Aliyeendesha mafungo haya ni Padre Vitus Sichalwe wa jimbo la Mbeya ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Kichungaji TEC. Baba Askofu alimshukuru Padre Vitus kwa kukubali mwaliko huu wa kuwasaidia mapadre katika tafakari ya mafungo yao. Mapadre pia walimshukuru sana padre V. Sichalwe na kumwomba awe tayari kuwashirikisha mengi aliyonayo. Aidha walimsifu sana kwa karama alio nayo katika fani ya kuendesha mafungo.

     Watawa wanaofanya kazi hapa jimboni Zanzibar walikuwa na siku ya tafakari 26 Novemba 2005 – iliyoongozwa na Monsinyo Julian Kangalawe. Kila mwaka watawa wote bila kujali shirika analotoka hukutana mara moja kwa mwaka kwa tafakari kama hii ingawa wanao utaratibu wa kila shirika kufanya mafungo ya mwaka kulingana na katiba zao.

     Mahafali katika Chuo cha Hekima Cheju yalifanyika 1.12.05 na shule ya Tomondo pia yalifanyika mahafali ya pili 3.12.2005 kwa wanafunzi waliohitimu darasa la saba. Mgeni rasmi katika mahafali yote alikuwa Makamu wa Askofu Padre Ambrose Mkenda.

     Mkutano Mkuu iliowajumuisha Mapadre, Masista, Halmashauri zote za Walei kuanzia ngazi ya Jimbo hadi Kigango, viongozi wa Vyama vya kitume na   Makatekista ulifanyika katika Kituo Machui tarehe 16 – 17 Desemba 2005. Mkutano huu ulihudhuruwa pia na Mhashamu Baba Askofu Augustino Ndelyakyama Shao na Uliendeshwa na Makale akishirikiana na Mkurugenzi wa Idara ya Kichungaji Padre Exupery Kilemi Lyimo. Mkutano huu  ulijadili maazimio yote ya kikao kilichofanyika mwezi Mei 10 – 20, 2005.

 Mhashamu Baba Skofu Augustino Shao aliadhimisha Misa ya Mkesha wa Krismasi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Zanzibar. Misa hii ilirekodiwa na kurushwa moja kwa moja (Live) na redio Maria. Watu wengi walihudhuria katika Misa hii iliyosisimua hasa kutokana na kwaya ya hapa Minara miwili iliyopamba ibada hii kwa nyimbo nzuri.

     Siku ya Krismasi 25.12.2005 Mhashamu Baba Augustino Shao aliadhimisha Ibada ya Misa katika Parokia ya Mpendae. Misa hii ilianza saa.4.00 za asubuhi na mara tu baada ya hitinisho la ibada ya Misa, Baba Askofu alitumbuizwa na watoto wa Haki na Amani waliotoa burudani ya igizo na nyimbo zinanazoendana na sikukuu ya Krismasi. Ibada ya Misa ya saa nne Mpendae ilirekodiwa pia na redio Maria (Live) na baada ya misa watu mbalimbali walikuwa na nafasi muafaka katika kutuma salamu zao za Krismasi. Watoto wa Haki na Amani nao walipata fursa ya kutuma salamu za Krismasi kwa watoto wenzao.

    Hii ni mara ya kwanza kwa redio Maria kurekodi Ibada ya Misa hapa Zanzibar baada ya matangazo yao kuanza kusikika hapa Unguja na Pemba toka Oktoba 2005.

    Sherehe za Watoto wa HAKI na AMANI zilifanyika katika shule ya Tomondo kuanzia Tarehe 27 Desemba2005 na kufikia kilele chake tarehe 28 Desemba 2005. Katika sherehe hizi zinazojulikana kama “Sherehe za Watoto wa Haki na Amani wakijumuika pamoja na Askofu,” watoto  kutoka Unguja na Pemba walijitokeza sana na kila kigango walionyesha vipaji vyao kwa njia ya nyimbo, ngonjera, maigizo, risala na ngoma. Watoto walifurahi sana kupata nafasi hii kwa siku mbili kusherekea sikukuu yao pamoja na Baba yao Askofu. Naye Mhashamu Baba Askofu Augustino Shao aliwasifu sana watoto kwa jinsi walivyoonyesha uwezo mkubwa katika kukuza vipaji vyao.

    Sherehe hizi ziliandaliwa na Sista mratibu wa watoto wa haki na Amani, Sista Rufina Funto akisaidiwa na masista wote wanaohusika na waototo pamoja na walezi katika vigango vyote. Sherehe hizi zilizinduliwa na Makamu wa Baba Askofu Padre Ambrose Mkenda kwa niaba ya Baba Askofu na hatimaye kufungwa na Baba Askofu katika siku ya kilele chake. Wengine waliohudhuria katika sherehe hizi ni Mkurugenzi wa PMS padre Exupery Kilemi, Chancellor wa Jimbo la Zanzibar Padre Cosmas Shayo pamoja na mapadre na masista kutoka parokia zote hapa Unguja. Baba Askofu alisisitiza tena kuhusu sherehe hizi kuwa ziwe zikifanyika kila mwaka.

    Siku ya 30.12.06 ilikuwa ni siku ya kumshukuru Mungu kwa yote aliyotujalia kwa mwaka wote 2005. Mapadre na Masista walishiriki katika siku hii ambayo Mhashamu Baba Augustino Shao aliwaalika kwa pamoja kwa nia ya kumshukuru Mungu kwa yale yote mema tuliyoweza kuyafanya katika mwaka wa 2005. Baada ya Mkutano Baba Askofu aliwaalika Mapadre wote na Watawa wote wa kike kwa mlo wa usiku. Katika siku hii ya kufana sana pia kulikuwa na wageni wanafunzi wa Shirika la Konsolata, kutoka Seminari ya Morogoro (Kola) ambao walishiriki pamoja nasi kwa hafla hii iliyoandaliwa na Baba Askofu.

    Mwisho wa mwaka 2005 na mwanzo wa mwaka 2006 Mhashamu Baba Augustino Shao alikuwa kisiwani Pemba kuwatakia waamini wa huko salamu za kheri kwa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya. Ziara ya Baba Askofu iliwatia moyo sana waamini wa parokia ya Wete na Chakechake hasa ukizingatia kuwa ni ziara ya mwisho wa mwaka 2005 na kuanza mwaka mpya 2006 pamoja nao. Baba Askofu aliwapatia baraka zote za mwaka mpya 2006.

    Baba Askofu alitoa ushemasi 6. Januari 2006 kwa Mashemasi wa Shirika la Roho Mtakatifu huko Usa River Arusha.  Kesho yake alielekea Maua kwa mafungo ya mwaka pamoja na mapadre wa shirika la Roho Mtakatifu. Mhashamu Baba Augustino Shao CSSp ni mtawa katika shirika la Roho Mtakatifu na aliwahi kuwa Mkuu wa shirika hilo kwa kanda ya Mashariki kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Zanzibar Mei 27.1997

    Bodi wa Maaskofu wanaohusika na seminari kuu za Taifa (Kibosho, Ntungamo,Kipalapala na Segerea) walikutana Tabora kwa mkutano kujadili kuhusu maswala mbalimbali kwa manufaa ya Waseminaristi na kuboresha seminari hizo kwa ujumla katika nyanja mbalimbali hasa kiroho, kitaaluma na kimaendeleo. Mhashamu Baba Askofu Augustino Shao ni miongoni mwa wajumbe wa bodi hiyo na  alijumuika na Maakofu wengine wa bodi huko  Tabora kwa kikao kilichofanyika tarehe 22. Januari 2006. Baada ya kuitembelea seminari kuu ya Tabora wajumbe walielekea Bukoba kutembelea seminari ya Ntungamo inayowaandaa wanafunzi wa falsafa.

Kuzinduliwa kwa Nyumba ya mapadre Tomondo

Kubarikiwa Kanisa jipya la Kizimbani

Tarehe 6. Augusti, 2006 Mhashamu Baba Askofu Augustine Shao wa Jimbo Katoliki la Zanzibar alibariki na kuzindua rasmi kanisa jipya la Kizimbani. Kanisa hili limejengwa na Kanisa la Kizimbani lilibarikiwa na Padre Paul Mallya wa Parokia ya Kiboje. Kizimbani ni kigango cha parokia ya Kiboje.

 

HISTORIA

ASKOFU

HABARI

OFISI

PAROKIA

SHULE

MASISTA

MAWASILIANO

KURASA 1

VIUNGANISHO